Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Vijana changamkieni fursa zitolewazo na serikali- Katambi


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amewataka Vijana nchini kuchangamkia fursa zinazotelewa na serikali Kwa lengo la kutatua suala la Ajira nchini.

Mhe.Katambi ameyasema hayo leo, tarehe 28 Oktoba, 2022 wakati wa Kongamano la Vijana kuhusu fursa zinazotelewa na Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi Vijana Ajira na Watu Wenye Ulemavu.

Mhe. Katambi amebainisha kuwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana Ajira na Watu Wenye Ulemavu, tayari Mhe.Rais Samia ametoa shilingi bilioni 1, ambapo kwa sasa kijana anaweza kukopa Kwa masharti nafuu akiwa peke yake badala ya kulazimika kuwa katika kikundi.

"Kuimarika kwa usimamizi wa mikopo ya asilimia 4 ya vijana inayotokana na mapato ya Halmashauri ni Moja ya hatua zilizofanywa na Mhe. Rais Samia kwa lengo kuwakwamua Vijana Kiuchumi "

Aidha, Mhe. Katambi amefafanua kuwa serikali inaendelea kutoa fursa za Mafunzo ya kuwajengea ujuzi vijana kupitia vyuo vya Elimu na vyuo vya mafunzo ya stadi na programu za kukuza ujuzi.

Ameongeza kuwa Halmashauri zote nchini zimeagizwa kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi, tayari maeneo yametngwa yenye ukubwa wa ekari 217,882.36 katika Mamlaka ya Serikali za mitaa 111, kwa ajili ya uwekezaji, wafanyabiashara wadogo na Watu Wenye Ulemavu katika kundi la vijana.

Aidha, Mhe.Katambi amesisitiza kuwa serikali inatambua mchango wa Vijana katika kujenga Uchumi, hivyo amewasihi Vijana kuchangamkia fursa zinazotelewa na serikali na kufanya kazi Kwa bidii