Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Vijana ni rasilimali muhimu inayoweza kuleta mageuzi ya kiuchumi: Mhe. Dkt. Samia


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema maeneo muhimu yanayoweza kusaidia kuboresha rasilimali watu kwa Afrika ni kutumia vijana tulio nao kama fursa pekee ya kuleta mageuzi ya kiuchumi.

Amesema hayo, wakati akihutubia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo tarehe 26 Julai, 2023, Jijini Dar es salaam.

Amesema katika kuwajengea maisha bora vijana nchi za Afrika ziongeze tija katika elimu na mafunzo yanayotolewa katika nchi hizo yawape uwezo vijana wa kukuza uchumi wa bara hilo.

Aidha, Rais Samia alitumia fursa hiyo kueleza programu maalum ya Bulding Better Tomorrow (BBT) inayotekelezwa na serikali kwa lengo la kuwawezesha vijana nchini kujishughulisha katika sekta ya kilimo, ufugaji, na uvuvi ili kutengeneza fursa za ajira.