Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waajiri Wasilisheni Michango ya Wafanyakazi kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii: Waziri Kikwete


Serikali imetoa wito kwa waajiri wote nchini,kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati kwenye mifuko ya Hifadhi ya jamii, ambayo ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ameyabainisha hayo leo Juni 18, 2025 Jijini Dar es Salaam katika Mkutano Mkuu wa 66 wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE).

Mhe. Kikwete amesema kuwa uwasilishaji wa michango hiyo utajenga misingi imara ya ajira zenya staha ikiwemo kuongeza uchumi Jumuishi unaozingatia utu,Usawa,na maendeleo ya pamoja ambayo yatajenga ustawahi kwa wafanyakazi wote ikiwemo uaminifu kazini.

Amesema Serikali iko tayari kuendelea kushirikiana katika kuboresha mazingira ya kazi na hasa katika kudumisha ushirikiano wa UTATU yani ATE, ILO, TUCTA kwa kuendelea kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya sasa na baadaye.

Aidha Waziri Kikwete amewahasa ATE kuwa na utendaji bora utakaotumika kama daraja huku akitoa wito kwa uongozi wa ATE kuendelea kuelimisha Waajiri nchini kuona umuhimu wa kujiunga na kujumuika pamoja katika Chama cha Wajiri.