Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Wadau wa Utatu watoa maoni mikataba sita ya ILO


Wadau wa Utatu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wametoa maoni kuhusu nchi kuridhia mikataba sita ya ILO.

Majadiliano hayo yameratibiwa na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Mashirika ya Maendeleo, leo jijini Dodoma.

Mikataba hiyo iliyojadiliwa na kutolewa maoni na wadau hao ni pamoja na; Mkataba wa Hifadhi ya Jamii; Mkataba wa Mafao ya Wafanyakazi wanaopata Majanga yatokanayo na Kazi; Mkataba wa Sera ya Ajira Mahala pa Kazi;

Aidha; mikataba mingine ni: Mkataba wa Mfumo wa kuhamasisha Masuala ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi; Mkataba wa Wafanyakazi wa Majumbani na Mkataba wa Wafanyakazi wa Majumbani.