Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​Wadau waipongeza serikali kuandaa mwongozo wa utambuzi wa mapema na afua stahiki kwa watoto wenye ulemavu


Wadau wameipongeza serikali kwa kuandaa Mwongozo wa Utambuzi wa Mpema na Afua Stahiki kwa Watoto Wenye Ulemavu ambao umechagiza kupunguza athari za ulemavu ukubwani ama kuondoa kabisa hali ya ulemavu.

Pongezi hizo zimetolewa wakati wa maadhimisho ya siku ya watoto wenye ulemavu wa vichwa vikubwa na mgongo wazi duniani (Spinal Bifida and Hidrocephalus Day) yaliyofanyika leo tarehe 25 Oktoba, 2023 jijini Dodoma.

Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri amesema utekelezaji wa mwongozo huo utaimarisha masuala ya upatikanaji wa haki, ulinzi na usalama kwa wototo hususani wenye ulemavu ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokutana na Watu Wenye Ulemavu Nchini Tarehe 16 Machi, 2022 Dodoma za kuwapatia afua stahiki watu wenye ulemavu.

Kwa upande wa Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Kizito Wambura ameeleza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Vyama vya Watu Wenye Ulemavu pamoja na Wadau mbalimbali kwa kuhakikisha masuala ya Watu Wenye Ulemavu yanapewa kipaumbele ili kukuza ustawi wa kundi hilo.