Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Wafanyakazi wa Hotelini 700 Mkoani Arusha kunufaika na mafunzo ya Ujuzi


Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeanza kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa wafanyakazi wa hotelini 700 mkoani Arusha ili kuwa na weledi wa kuhudumia watalii wanaokuja nchini.

Mafunzo hayo yanatolewa kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi iliyopo chini ya ofisi hiyo ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kupaisha sekta ya utalii nchini kwa kuhakikisha watalii wanahudumiwa kwa weledi na ujuzi stahiki.

Akifungua mafunzo hayo Julai 24, 2023 jijini Arusha, Mkurugenzi Msaidizi wa Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi hiyo, Robert Masingiri, amesema mafunzo hayo ni ya wiki moja na yamegusa idara zote za hotelini ili watalii wanaokuja wapate huduma bora.

“Lengo la serikali pamoja na elimu mliyonayo inawaongezea ujuzi zaidi wa kuhudumia hawa wageni wetu ili kuvutia wengi zaidi kuja nchini na kufikia idadi ya watalii milioni tano ifikapo mwaka 2025,”amesema.

Amewahimiza washiriki kuzingatia mafunzo hayo ambayo yamebeba ujuzi wa maeneo mbalimbali.