Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Wahitimu 21,280 Wamenufaika na Programu ya Taifa ya Mafunzo ya Uzoefu wa Kazi


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Serikali ilianza rasmi kuratibu utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Mafunzo ya Uzoefu wa Kazi kwa wahitimu (internship) mwaka 2019/2020.

Aidha, tangu kuanza kwa utekelezaji wa programu hiyo jumla ya Wahitimu 21,280 wamenufaika ambapo wanaume ni 11,281, wanawake 9,999 na Miongoni mwa wanufaika hao jumla ya Wahitimu 3,772 wamepata kazi Serikalini, Sekta Binafsi na nje ya Nchi.

Mhe. Ndejembi amebainisha hayo leo Aprili 18, 2024 Bungeni Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Shally Joseph Raymond lililohoji, Wahitimu wangapi wa Vyuo wanafanya kazi ya kujitolea na wangapi wameajiriwa na kujiajiri baada ya kujitolea.