Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Wakufunzi na Watendaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu wapatiwa mafunzo ya Stadi za Maisha "Life Skills"


Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana inaratibu Programu ya Stadi za Maisha (Life Skills) kwa lengo la kuwawezesha vijana mbinu zitakazowapa uwezo wa kujiimarisha kiakili na kiujuzi ili kumbambana na uhalisia wa Maisha ya kila siku.

Idara hiyo yenye dhamana ya maendeleo ya vijana nchini imetoa mafunzo kwa wakufunzi na watendaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu ambao pia ni Wawezeshaji wa Stadi za Maisha Kitaifa (National Facilitators) ili kuhakikisha elimu hiyo inajumuishwa kwenye afua na program za kushughulikia changamoto za vijana wenye Ulemavu.

Aidha, Mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha wakufunzi na watendaji hao elimu ya stadi za maisha inawafikia vijana wenye Ulemavu ili waweze kujitambua, kuwa na uthubutu na kufanya maamuzi sahihi na kuepuka vishawishi pamoja na mazingira hatarishi.

Vile vile, Stadi hizo za Maisha zitawaongezea hali bora ya vijana nchini na kuwawezesha kuwa watu wenye tija katika jamii zao, sambamba na kumwezesha kijana asiye na Ulemavu na wenye Ulemavu kupata majibu kwa maswali makuu matatu (3) ya maishani ambayo ni Mimi ni nani; Ninataka kwenda wapi maishani; na Nitafikaje huko ninakotaka kwenda.