Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Wakulima wa Zabibu wapongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kuwapa Ujuzi


Wakulima wa zabibu wa Mvumi jijini Dodoma wameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuandaa mafunzo ya ukuzaji ujuzi yaliyolenga kuboresha mbinu za kilimo na kuongeza tija katika uzalishaji wa zao hilo.

Aidha, mafunzo hayo yamewanufaisha wakulima kwenye maeneo yenye shughuli za kilimo cha zabibu kwa kuwaleta pamoja wakulima na wadau kwa lengo la kubadilishana maarifa na teknolojia mpya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima walioshiriki, wamesema mafunzo hayo yamewasaidia kuelewa mbinu bora za upandaji, utunzaji wa mashamba na kutafuta masoko ya zao hilo la zabibu, jambo ambalo litasaidia kuongeza kipato cha wakulima na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika maeneo yao.

Mmoja wa wakulima kutoka Mkoa wa Dodoma alisema, “Mafunzo haya yametufungua macho. Tumejifunza jinsi ya kutumia mbolea kwa usahihi, kudhibiti magonjwa na hata kutafuta masoko ndani na nje. Tunashukuru sana serikali kwa kututambua na kutuwezesha ujuzi huu.” (Tuandike jina la Mmoja wa Wakulima waliotoa shukrani.......)

Kwa upande wake, (Cheo cha Afisa Bw. Denis Assey.....) amesema Ofisi ya Waziri Mkuu imeendela kutoa mafunzo ya kuongeza ujuzi kwa Wafanyakazi waliopo katika sekta mbalimbali nchini kupitia programu ya Taifa ya ukuzaji ujuzi ili kuhakikisha wafanyakazi wanapata maarifa ya kisasa yatakayowasaidia kukabiliana na changamoto na kuzalisha kwa tija na ubunifu.

Vike vile, amesema mafunzo hayo waliyopatiwa wakulima na wadau wa Zabibu ni sehemu ya jitihada za serikali za kuinua sekta ya kilimo na kuhakikisha wakulima wanakuwa na uwezo wa kushindana katika soko la ndani na la kimataifa.Wakulima wa