Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Kikwete abainisha mabo 5 ya Serikali ya Awamu ya Sita katika Kuimarisha Uchumi wa Vijana na Wenye Ulemavu


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu kazi – Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amebainisha mambo 6 yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwawezesha vijana na watu wenye ulemavu ili waweze kujiinua kiuchumi.

Akiyabainisha mambo hayo leo Juni 16, 2025 katika Kongamano la 9 la ununuzi wa umma la mwaka 2025 Jijini Arusha, Mhe.Kikwete amesema utekelezaji wa agizo la kisheria la kutenga asilimia 30 ya zabuni za ununuzi wa umma imeongeza ushiriki wa vijana na watu wenye ulemavu katika michakato ya zabuni katika Mwaka wa Fedha 2023/24 ambapo Jumla ya Vikundi vya Vijana119 vilipata Tuzo za zabuni zenye thamani ya shilingi Bilioni 4.02.

Amebainisha pia utekelezaji wa mpango wa asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, suala hilo limeongeza usatwi wa makundi hayo, ambapo Katika mwaka 2024/25, zaidi ya Shilingi bilioni 82.84 zilitolewa kwa vikundi 8,275 vya wanawake, vijana na wenye ulemavu.

Mhe. Kikwete amebainisha jambo lingine kuwa ni Kuimarisha Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa kutoa mitaji nafuu kwa vijana waliojiajiri au wanaoanzisha biashara ambapo Katika mwaka 2022/2023 na 2023/24, Shilingi bilioni 3.1 zilitolewa kwa kufadhili miradi 141 ya vijana.

Suala jingine liloimarisha ustawi wa vijana na watu wenye ulemavu ni Kukamilisha na kuanza kutekeleza Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana (2007); Toleo la 2024; Mwongozo wa Utekelezaji, Ujumuishwaji na Uimarishaji wa Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu Tanzania (2022); Mpango Kazi wa Taifa wa Teknolojia Saidizi (2024-2027).

Mhe. Kikwete amesisitiza kuwa vijana wameendelea kunufaika kupitia programu ya Taifa ya ukuzaji Ujuzi ambapo jumla ya vijana 154,778 wamenufaika kupitia program hiyo.

Kauli mbiu ya Kongamano hilo ilkuwa ni; Ununuzi wa umma Kidijitali kwa maendeleo Endelevu: Ukuzaji wa kampuni za wazawa na makundi maalum kwa ukuaji wa Uchumi Jumuishi.