News
Waziri Kikwete: Ajira za Vijana zaidi ya 2000 kuzalishwa maonesho ya fursa za Ajira Tanzania na China
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu amesema zaidi ya ajira 2000 zinategemewa kuzalishwa kutokana na maonesho ya Fursa za ajira kwa Vijana kati ya Tanzania na China.
Mhe. Kikwete amesema maonesho hayo ni kati ya hatua za serikali ya Awamu ya Sita katika kutatua changamoto ya Ajira nchini, ambapo kupitia maonesho hayo makampuni ya China yanayofanya kazi hapa nchini yanaonesha mahitaji yao ya ujuzi wanaohitaji ili vijana wakitanzania weweze kuchangamkia fursa hizo. Hivyo vijana wenye sifa za mahitaji ya makampuni hayo watapata kuajiriwa.
Mhe.Kikwete amebainisha hayo maonesho leo tarehe 28 Juni 2025 mara baada ya kufungua maonesho hayo yanayoendelea katika Viwanja vya Chuo kikuu Dar es salaam ambapo ameongeza kuwa Tanzania na China wamekubaliana katika shughuli za makampuni yao hapa nchi kuwapa nafasi vijana wazawa wenye sifa wanazohitaji .
Katika hatua nyingine Mhe.Kikwete amewataka vijana kujitokeza kwa wingi kutembelea maonesho hayo ili kuchangamkia fursa hizo za ajira.Aidha amewahakikishia watanzania kuwa serikali kupitia ofisi hiyo itaendelea kuratibu kwa tija masuala ya ajira nchini .