Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​WAZIRI NDALICHAKO AKAGUA MAANDALIZI YA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU


WAZIRI NDALICHAKO AKAGUA MAANDALIZI YA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU

Waziri wa Nchi ofisi ya waziri Mkuu, kazi, vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ametembelea na kukagua shughuli za mbio za maandalizi ya kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Kagera, zinazotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 6 Oktoba, 2022 hadi siku ya kilele tarehe 14 Oktoba, 2022.

Akizungumza mjini Bukoba, tarehe 7 Septemba, 2022 mara baada ya kukagua maandalizi ya kilele cha Mbio hizo katika uwanja wa Kaitaba amebainisha kuwa katika kilele cha mbio za Mwenge, Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Mhe. Ndalichako ameupongeza uongozi wa mkoa huo kwa maandalizi wanayo endelea nayo ambapo amekagua mafunzo ya Halaiki, Uwanja wa Kaitaba ambapo zitafanyika shughuli za kilele cha Mbio za Mwenge na Viwanja vya Gymkhana ambapo yatafanyika maonyesho ya wiki ya Vijana.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila amebaimisha kuwa vijana wa Albert Chalamila ameeleza kuwa mkoa umejizatiti katka kuhakikisha sherhe za kilele cha mbio za Mwenge ziweze kufana ambapo kabla ya kilele hicho kutakuwepo na Maonesho ya wiki ya Vijana kuanzia tarehe 14 Oktoba 2022 hadi tarehe 14 Oktoba 2022.

Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022 zinaongozwa na vijana sita kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, ambao wanalojukumu la kuukimbiza Mwenge wa Uhuru katika mikoa 31 na halmashauri 195 nchini kwa siku 195.

Mbio hizo zimeendelea kuelimisha na kuihamasisha jamii ya Watanzania kuhusu umuhimu na uzingatiaji wa Lishe bora, Mapambano dhidi ya Rushwa, Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za kulevya pamoja na Mapambano dhidi ya Malaria.

Shughuli za Mbio za Mwenge nchini huratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana, ambapo huu ni mwaka wa 30 tangu serikali ianze kuratibu na kusimamia Mbio za Mwenge. Lengo la serikali kusimamia mbio za Mwenge ni kuwakilisha wananchi wote bila kujali itikadi zao za kisiasa, dini, rangi na ukabila.