Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ndalichako atoa somo kwa Vyama vya Wafanyakazi


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amevitaka Vyama vya Wafanyakazi nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba, utaratibu na miongozo waliyojiwekea.

Waziri Ndalichako amesema hayo Disemba 15, 2022 kwenye mkutano mkuu wa Chama cha Walimu (CWT), uliofanyika jijini Dodoma.

Ameeleza kuwa ni muhimu vyama hivyo vikaepusha migogoro mahala pa kazi huku akiwasihi waajiri kuvitambua na kuviheshimu Vyama vya Wafanyakazi.

"Baadhi ya waajiri wamekuwa ni kikwazo katika vyama vya wafanyakazi kufanya kazi zao naomba watambua vyama vya wafanyakazi vipo kwa mujibu wa sheria na ni daraja kati ya waajiri, serikali na wafanyakazi, kwa hiyo wawape nafasi wafanye kazi zao, waruhusu mabaraza ya wafanyakazi yafanye kazi kwa mujibu wa taratibu,"

"Vyama vya Wafanyakazi ni kiungo mathubuti kati ya wafanyakazi na waajiri mahala pa kazi, hivyo vikitekeleza majukumu yao kwa weledi na kadri ya miongozo iliyojiwekea kwenye katiba na kanuni za kuendesha vyama daima kutakuwa na mahusiano mema kwenye maeneo ya kazi," amesema

Alibainisha kuwa milango ya Serikali ipo wazi wakati wote kuhakikisha inafanyia kazi changamoto za wafanyakazi kwa wakati ili kuwa na tija na ustawi mahala pa kazi.