Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ndalichako Azindua Huduma Maalum kwa Wastaafu NMB Hekima Plan


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amezindua mpango maalum unaoratibiwa na Benki ya NMB wenye masuluhisho mahususi kwaajili ya kuwahudumia Wastaafu na Wastaafu watarajiwa unaoitwa NMB Hekima Plan wenye Kauli Mbiu “Staafu Kifahari”

Akizungumza katika warsha iliyowakutanisha Wastaafu na Wastaafu watarajiwa zaidi ya 400 jijini Dodoma kwa ajili ya kuwaelimisha na kuwaandaa kukabiliana na changamoto za maisha baada ya ajira. Profesa Ndalichako ameipongeza Benki ya NMB kwa kuja na utaratibu huu ambao lengo lake kubwa ni kusaidia kuenzi mchango mkubwa wa wastaafu katika ujenzi wa taifa.

Mkuu wa Idara ya Biashara ya Serikali wa benki hiyo, Bi. Vicky Bishubo alieleza kuwa, utaratibu huo wa wastaafu watapewa pia elimu ya ustawi wa afya na usalama wa fedha zao huku wakionyeshwa fursa mbalimbali za uwekezaji. Lakini pia, NMB Hekima Plan ina bima za afya na mali za gharama nafuu na bei shindani sokoni.

Zipo pia Akaunti maalumu zisizokuwa na makato ya mwezi ambazo zinampa nafasi mstaafu kupata mkono wa pole wa hadi Tsh milioni 2 endapo yeye au mwenza wake atafariki na kumwezesha kupata kiasi kama hicho akipata ulemavu wa kudumu.