Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ndalichako: Bil. 1 za Mfuko wa Vijana Zimekopeshwa kwa Walengwa


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, amesema hadi Juni 2022 fedha zilizotengwa kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana Sh.Bilioni moja zimekopeshwa kwa walengwa.

Akichangia jana taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria bungeni, Prof.Ndalichako, amesema ofisi yake itahakikisha inatoa elimu ya kutosha kwa vijana kuhusu mfuko huo.

“Mwongozo wa namna ya kupata mikopo unapatikana katika halmashauri zote nchini, tumeboresha na tumeainisha kiwango cha juu cha kupata mikopo kutoka Sh.Milioni 10 hadi 50, tumelegeza masharti kijana anaweza kwa kikundi au mmoja mmoja,”amesema.

Kuhusu mwongozo wa ujumuishaji na uimarishaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu, Mhe.Ndalichako amesema elimu itatolewa ili taasisi za serikali na zisizo za serikali zitekeleze kwa ufanisi.

Kadhalika, amesema Ofisi yake kwa kushirikiana na TAMISEMI kuwa na mfumo endelevu wa kuweka taarifa za watu wenye ulemavu kama kamati hiyo ilivyoshauri.

Akizungumzia sera ya taifa ya vijana, amesema kwasasa maoni yanakusanywa na hadi Desemba mwaka 2023 wanatarajia kukamilisha mapitio ya sera hiyo.