Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

WAZIRI Ndejembi atembelea OSHA


* Asisitiza Uwekezaji katika TEHAMA Kurahisisha Utendaji Kazi

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi ameitaka Menejimenti ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kuwekeza zaidi katika mifumo ya kidijitali ili kurahisisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi.

Mhe. Ndejembi ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipotembelea taasisi hiyo kwa lengo la kujifunza namna OSHA inavyotekeleza majukumu yake.

Akizungumza na menejimenti hiyo, Mhe. Ndejembi ameitaka OSHA pia kuongeza jitihada za kuwaelimisha na kuwahamasisha wadau wa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi ili waweze kutekeleza sheria na miongozo mbalimbali ya usalama na afya kwa hiari.

“ Nimejifunza mengi kutokana na wasilisho la Mtendaji Mkuu hivyo niwatake menejimenti kuwekeza zaidi katika mifumo ya TEHAMA pamoja na kubuni mikakati ya kuongeza uelewa miongoni mwa wadau wenu na wananchi kwa ujumla ambao uelewa wao kuhusu kazi zinazofanywa na taasisi hii ni mdogo,” amesema Mhe. Ndejembi.

Kwa upande mwengine, Mhe. Ndejembi ameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Mashirikiano baina ya OSHA na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) yatakayowezesha Taasisi hizo mbili kushirikiana katika suala la utoaji elimu ya usalama na afya kwa wanachama wa TUGHE nchini.

Katika ziara hiyo Mhe Waziri Ndejembi ameambatana na Kamishna wa Kazi, Bi Suzan Mkangwa.