Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ridhiwani Kikwete Ashiriki Mkutano wa Vijana Nchini China


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameshiriki katika Mkutano wa 14 wa Vijana wa Dunia uliofanyika katika Mji wa Suzhou nchini China.

Akizungumza katika mkutano huo, Mhe. Ridhiwani Kikwete amebainisha hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Mhe. Rias Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwawezesha vijana wa nchini Tanzania.

Aidha, amesema baadhi ya hatua hizo ni pamoja na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu, kutoa fursa ya asilimia 30 ya manunuzi ya umma kwa vikundi hivyo pamoja na utoaji wa mikopo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi na programu nyingine.

Vile vile, alieleza kuwa Serikali imeendelea kuweka msisitizo mkubwa katika Sera, Sheria, na Mipango inayolenga kukuza maendeleo ya vijana.

Kwa upande mwengine, alieleza kuhusu Sera mpya ya Vijana na utekelezaji wa programu za maendeleo kama BBT – Kilimo, Mifugo na Madini zimekuwa na mafanikio makubwa na zimechangia kuongeza ushiriki wa vijana katika maendeleo ya taifa.

Mkutano huo umehudhuriwa na washiriki kutoka mataifa mbalimbali na umetoa fursa kwa viongozi kubadilishana uzoefu mbinu bora za kushughulikia changamoto za vijana, kukuza ajira na ujuzi pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kwa maendeleo endelevu.