Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

Announcement

Announcement for Apprenticeship Opportunity


 1. Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu inatekeleza Programu ya Kukuza Ujuzi Nchini inayowezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira. Ofisi imeingia makubaliano vyuo mbalimbali kutoa mafunzo mafunzo ya ufundi stadi kukuza ujuzi na stadi za kazi kwa vijana. Miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa ni Ubunifu wa Mitindo na Ushonaji Nguo, Ufundi Bomba, Uashi, Useremala, Uchomeleaji na Uungaji vyuma, Upakaji rangi na maandishi ya alama, Utengenezaji wa vipuri vya mitambo, Ufundi Magari na Mitambo, Umeme wa Majumbani na Viwandani, TEHAMA, Umeme wa Magari, Huduma za Hoteli na Utalii, Ukataji Madini ya Vito na Kilimo.
 2. Hivyo, tunapenda kuwatangazia vijana wa Kitanzania wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 wanaopenda kujiunga na mafunzo katika mojawapo ya fani zilizoorodheshwa hapo juu wafike katika vyuo vilivyoainishwa na Tangazo hili hapa chini ili kuchukua fomu ya kuomba kujiunga na mafunzo. Serikali itafadhili ada ya mafunzo kwa asilimia 100. Mwanafunzi / mzazi / mlezi atagharamia gharama nyingine zikijumuisha nauli ya kwenda chuoni na kurudi nyumbani. Mafunzo yatakayotolewa ni ya kutwa hivyo mwombaji anashauriwa kuomba mafunzo haya katika chuo kilicho katika Mkoa anaoishi.
 3. Maombi yawasilishwe kuanzia tarehe 01/11/2023 hadi tarehe 14/11/2023 yakiambatana na nyaraka zifuatazo:
 4. i. Barua ya maombi ya mafunzo;

  ii. Nakala ya Cheti cha kuzaliwa;

  iii. Nakala ya Cheti cha elimu uliyohitimu ;

  iv. Kitambulisho cha uraia / kadi ya mpiga kura (Kwa wenye miaka 18 na kuendelea);

  v. Barua ya utambulisho kutoka Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji anakoishi mwombaji; na

  vi. Picha nne za paspoti (ziandikwe majina matatu ya mwombaji kwa nyuma).

  4. Sifa za kujiunga na mafunzo haya ni:

  i.Elimu ya msingi au zaidi kwa fani za ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo, ufundi bomba, ujenzi, useremala, uchomeleaji na uungaji vyuma, upakaji rangi na maandishi ya alama;

  ii.Elimu ya kidato cha nne na kuendelea kwa fani nyingine zilizobaki zikijumuisha fani ya utengenezaji wa vipuri vya mitambo, ufundi magari, umeme wa majumbani na viwandani, TEHAMA, umeme wa magari na umeme wa jua (solar);

  iii.Awe Mtanzania;

  iv.Awe na umri kati ya miaka 15 – 35;

  v.Awe mwenye afya njema;

  5. Vijana wa Kike na Vijana Wenye Ulemavu wanasisitizwa kuomba fursa hizi na watapewa kipaumbele katika nafasi za mafunzo haya;

  6. Maombi yachukuliwe na kuwasilishwa kwenye vyuo vilivyo katika Mkoa wako ambavyo vimekubaliwa na Serikali kutoa mafunzo haya; na

  7. Watakaokidhi vigezo na sifa tu ndio watakaochanguliwa

  Tangazo hili linapatikana katika Tovuti ya Ofisi (www.kazi.go.tz)

  IMETOLEWA NA:

  KATIBU MKUU

  01/11/2023

NB: Fomu za maombi zinapatikana katika vyuo vyote vilivyopitishwa na Serikali kutoa mafunzo haya.


VYUO VILIVYOKUBALIWA KUTOA MAFUNZO YA UANAGENZI

NA

MKOA

WILAYA

JINA LA CHUO

FANI

1

Arusha

Arusha Jiji

Don bosco KII - TECH

Umeme jua

ufundi umeme

Karatu

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mto wa Mbu

Uongozaji Watalii

Ufundi Bomba

Umeme wa Majumbani

2

Dar es salaam

Temeke

Dsm RVTSC

Ufundi Magari

Ufundi wa kutengeneza vifaa kutumia Aluminium

Ufundi Bomba

Umeme wa Majumbani

Uchomeleaji na Uungaji vyuma

Ukarabati wa bodi za magari

Ufundi Umeme wa Magari

Ushonaji

Kinondoni

Don bosco Oysterbay VTC

Ufundi magari

Useremala

Uchomeleaji na uungaji vyuma

Uchorongaji vipuri

Ushonaji

3

Dodoma

Dodoma

Instistute of Heavy Equipment and Technology (IHET)

Ufundi wa mitambo

Uchomeleaji na uungaji vyuma

Umeme wa magari

Don Bosco Dodoma Technical Institute

Useremala

Ufundi bomba

Uashi

Uchomeleaji na uungaji vyuma

Ufundi magari

Uchorongaji vipuri

Ufundi umeme

Ushonaji

Umeme jua

4

Geita

Geita

Geita VTC

Umeme Majumbani

Ufundi Magari

Ufundi Bomba

Uashi

5

Iringa

Iringa

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Ilula

Umeme wa majumbani

Useremala

Ushonaji

Uchomeleaji na uungaji vyuma

Mufindi

Mafinga Lutheran Vocational Training Centre

Ufundi magari na Mitambo

Uchomeleaji na Uungaji wa Vyuma

Useremala

Ushonaji

Kilolo

RDO Kilolo VTC

Umeme wa Majumbani

Upishi

Ushonaji

Useremala

Uashi

6

Kagera

Biharamulo

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Rubondo

Umeme wa majumbani

Ufundi magari

Ushonaji

Uashi

Misenyi

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Gera

Ufundi umeme

Uashi

Kilimo

7

Katavi

Mpanda

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Msaginya

Umeme wa Majumbani

Useremala

Ushonaji

Kilimo

8

Kigoma

Kasulu

Kasulu DVTC

Ufundi umeme wa majumbani

Uashi

Ufundi Magari

Ushonaji

Kasulu

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kasulu

Ufundi umeme wa majumbani

Uchomeleaji na uungaji vyuma

Umeme wa magari

Ufundi bomba

Ushonaji

Ufundi magari

Kakonko

Chuo cha Ufundi Stadi JKT Kasanda

Ufundi bomba

Ufundi umeme

Upishi

Ushonaji

Ufundi magari

Kigoma Vijijini

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kihinga

Umeme wa majumbani na viwandani

Uashi

Ushonaji

9

Kilimanjaro

Moshi Vijijini

Marangu School of Tourism and Vocational Training

Kuongoza watalii

Upishi

Huduma za kupokea wageni

Huduma za vyakula na vinywaji

Rombo

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mamtukuna

Uashi

Useremala

Ufundi Magari

Umeme wa Majumbani

10

Lindi

Kilwa

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko

Umeme wa majumbani

Ushonaji

Ufundi Magari

Kuongoza Watalii

Ruangwa

Ruangwa DVTC

Ufundi umeme wa majumbani

Uashi

Ushonaji

Ufundi magari

11

Manyara

Mbulu

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Tango

Umeme wa majumbani

Useremala

Ufundi magari

Ushonaji

Uashi

12

Mara

Musoma

St. Anthony Vocational Training Centre

Ushonaji

Ufundi magari

Uchomeleaji na uungaji vyuma

Umeme wa magari

13

Mbeya

Mbeya Mjini

Chuo cha Ufundi Magereza Ruanda

Useremala

Uashi

Umeme wa majumbani

Ushonaji

Uchomeleaji na uungaji vyuma

14

Morogoro

Morogoro

Lakewood Training Institute

Umeme wa majumbani

Kuongoza watalii

15

Mtwara

Masasi

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Masasi

Umeme wa majumbani

Ushonaji

Ufundi bomba

Uashi

Uchomeleaji na uungaji vyuma

16

Mwanza

Ilemela

Mwanza RVTSC

Uchomeleaji na Uungaji vyuma

Ufundi Umeme wa Majumbani

Useremala

Ufundi wa uchanganyaji na upakaji rangi

Ginnery Fitting

Ufundi magari

Ufundi Bomba

Sengerema

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Sengerema

Ufundi Umeme

Uchomeleaji na Uungaji vyuma

Ufundi magari

Ushonaji

Uashi

17

Njombe

Njombe

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Njombe

Umeme wa majumbani na viwandani

Ushonaji

Ufundi magari na mitambo

Uchomeleaji na uungaji vyuma

Uashi

18

Pwani

Kibaha

Pwani RVTSC

Ufundi umeme wa majumbani

Useremala

Ufundi umeme wa magari

Utengenezaji wa friji na Viyoyozi

Ushonaji

Ufundi magari

19

Rukwa

Sumbawanga

LAELA AGRICULTURE VTC

Kilimo cha mbogamboga (Horticulture)

Ufugaji (Animal Husbandry)

Sumbawanga

Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST - Rukwa)

Uchomeleaji na Uungaji vyuma

Uashi

Ufundi bomba

Ufundi Umeme wa Majumbani na Umeme Jua

20

Ruvuma

Mbinga

Chuo cha Ufundi Stadi Mpapa

Useremala

Ushonaji

Umeme

Uchomeleaji

Songea vijijini

Peramiho Vocational Training Center

Ushonaji

Ufundi Bomba

Useremala

Ufundi Magari

Umeme wa Majumbani

21

Shinyanga

Kahama

Hill Forest College - Kahama

Front Office Operations

22

Simiyu

Bariadi

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bariadi

Umeme wa majumbani

Ufundi magari

Uchomeleaji na uungaji vyuma

Ushonaji

Uashi

Useremala

23

Singida

Singida Mjini

Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu Sabasaba

Umeme wa Majumbani

Ushonaji Nguo

Ususi na Urembo

Uchomeleaji

Uokaji keki na mikate

Singida mjini

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Singida

Ufundi umeme

Ufugaji

Useremala

Ushonaji

Ufundi magari

24

Tabora

Urambo

Urambo DVTC

Ushonaji

Uashi

Ufundi umeme wa majumbani

Nzega

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mwanhala

Umeme wa majumbani

Ufundi magari

Ushonaji

Uashi

25

Tanga

Lushoto

St. Patrick's Vocational Training Centre

Ufundi Magari

Useremala

Ushonaji

Umeme wa magari

Umeme wa majumbani

Handeni

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Handeni

Ufundi umeme wa majumbani

Ufundi magari

Upishi

Ushonaji

Uchomeleaji na uungaji vyuma